Rais Vladimir Putin wa Russia Februar 24 mwaka huu aliamuru kushambuliwa Ukraine na kuwataka wananajeshi wa Ukraine kuweka chini silaha zao na kurejea majumbani. Ni kwa muda mrefu sasa Ukraine inasisitiza kupewa uanachama ndani ya muungano wa NATO ili kudhaminiwa usalama wake lakini muungano huo wa kijeshi wa nchi za Magharibi unapeleka misaada ya kifedha na kisilaha kutoka kwa Ukraine pekee katika vita vinavyoendekea kati ya Russia na nchi hiyo.
Wakati huohuo Russia na Belarus ni washirika pia katika Taasisi ya CSTO; na zinashiriki pia katika maneva ya pamoja ya kijeshi yenye lengo la kuiunganisha miundo ya kijeshi ya nchi mbili hizo kwenye serikali ya muungano.
Shirika la habari la Sputnik limearifu kuwa, Dmitry Peskov Msemaji wa Kremlin amesema kuwa: tuko pamoja katika majukumu yetu ya kiulinzi; kwanza katika fremu ya Muungano wa Russia na Berus na pili katika kalibu ya Taasisi ya CSTO. Peskov ameongeza kusema kuwa, kwa msingi huo pande mbli za Russia na Belarus zinashirikiana kikamilifu; na hakuna yoyote anayepasa kuhoji ukweli huu.
342/